Connect with us

Business

Maisha Yazidi Kuwa Magumu Kenya.

Published

on

Wakenya wajiandae na hali ngumu inayofwata Kenya baada ya kupandishwa kwa bei ya vitu.Sasa taasisi ya Energy,Petroleum and Regulatory Authority inayofahamika kama “EPRA” imetangaza ya kwamba wanapandisha bei ya petroli kwa shillingi tatu kwa kila lita.

Dizeli nayo imepanda shillingi 0.39ksh kwa kila lita, mafuta taa pekee ndio yameshuka bei kwa shillingi 0.34 kwa kila lita.

Baadhi Ya Bei

Nairobi watalazimika kulipa Shillingi 115.10 kwa kila lita ya petrol na shillingi 104.76 kwa dizeli na shillingi 104.28 kwa mafuta ya taa.

Mombasa watalazimika kulipa shilllingi 115.10 kwa petroli,shillingi 104.76 kwa dizeli na shilllingi 104.28 kwa kila lita ya mafuta taa

Nakuru watalazimika kulipa shilllingi 115.57 kwa petroli,shillingi 105.45 kwa dizeli na shilllingi 104.98 kwa kila lita ya mafuta taa

Kisumu watalazimika kulipa shilllingi 116.56 kwa petroli,shillingi 105.97 kwa dizeli na shilllingi 105.97 kwa kila lita ya mafuta taa

“This month’s changes are as a consequence of average landed cost of imported Super Petrol increasing by 4.54% from US$514.72 per cubic metre in April 2019 to US$538.08 per cubic metre in May 2019, “Diesel increasing by 0.52% from US$533.07 per cubic meter to US$535.84 per cubic meter and Kerosene decreasing by 0.43% from US$535.17 per cubic meter to US$532.89 per cubic meter,” walisema EPRA

Bei za mafuta ziliathirika siku ya Ijumamosi June tarehe 15 na zinategemewa kwenda kwa mfumo huo mpaka July 14 2019.

Kama inavyofahamika inapopanda bei ya mafuta itapanda bei ya vitu vyote hapa Kenya kama vyakula na vyenginevyo vingi tu.Kwa sababu mashine na vyombo vya usafiri ambazo zinazoandaa na kukufikishia wewe mtumiaji vyote vinatumia mafuta.

Mfumuko wa bei ulipanda ambao sasa ni asilimia 6.85 April toka asilimia 4.53 iliokuwa ni march ambayo ilikuwa piya tayari imepanda kutokana na Februari ambayo ilikuwa asilimia 4.14

Kulingana kwa vitu kupanda bei kila siku maisha yatazidi kuwa kwenye hali ngumu kuliko yalivyokuwa mwanzo

I am a swahili blogger and a content creator for mgahawani.com Get me through yusuf@mgahawani-5ddae7.easywp.com

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Like Us on Facebook

Copyright © 2020 Mgahawani Media.