Connect with us

Sports

Mungu pekee ndie atakae muamulia Sadio Mane na chama lake kuchukua ubingwa UEFA na Ballon D’or.

Published

on

Tukiwa tumebakiwa na siku 19 pekee za kuisubiria Fainali ya klabu bingwa Ulaya (UEFA) siku zinazidi kuendelea kupungua huku kila mchezaji akiwa katika juhudi za kupasha misuli na wengine wakiona haitoshi, ila ni kuingia katika ibada kuu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Inafahamika wapo wachezaji wengi ambao katika misimu mbali mbali kama Pogba, Mesut Ozil, Riyad mahrez na Mohammed Elneny walishawahi kujianika wakiwa katika sehemu tukufu za ibada. Katika video ilioenea mitandaoni ya mnamo mwaka 2018, mtu mmoja alibahatika kuwepo ndani ya mskiti alioingia kusali staa huyo wa Liverpool, na hii ilileta maana kubwa kuwa staa huyo ni mtu wa ibada sana mara kwa mara pia akiingia uwanjani na akifunga mabao pia ushangiliaji wake akisujudu. Mbali na kumshukuru Mungu kwa tuzo ya ufungaji bora, bado staa huyo anazidi kumuomba Mola wake akiwa katika funga ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ili apate mengi zaidi.

Sadio Maneakijumuika na waislamu wenzie kusali katika msikiti mmoja ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Sadio mane pia yupo katika kinyang’anyiro cha wale watu watano wanaotarajiwa kuwania tunzo ya Ballon d’or pamoja na orodha ndefu ya kina Lionnel Messi, Van dijk, Raheem sterling na Aubameyang Cristiano Ronaldo na kadhalika. Lionel Messi pamoja na kufanya vizuri msimu huu kando na kutolewa kwenye michuano ya UEFA, wengi wamebashiri kuwa yeye na Cristiano kuna uwezekano mkubwa kuwa wasiweze kujinyakulia tuzo hiyo na baadae tuzo hiyo ikaangukia mikononi mwa wachezaji hao wa Ligi kuu ya Uingereza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Like Us on Facebook

Copyright © 2020 Mgahawani Media.