Connect with us

ENTERTAINMENT

Msanii Yemi alade afuata nyayo za Diamond Platnumz kumshirikisha staa Rick Ross.

Published

on

Yemi Eberechi Alade aka Yemi Alade ambae ni miongoni mwa wasanii maarufu barani Afrika kutokea Nigeria, aliwahi kutamba sana na nyimbo yake Johny na kuweza kumtambulisha kimataifa zaidi kando na kazi zake kubwa alizo fanya na kumuweka kileleni. Msanii huyi mwenye sauti nyororo kiuwezo wa kuimba na vionjo flani vya Rap kudhihirisha ubunifu wake ameweza kuwavutia wadada wengi sana kwa nyimbo na mitindo hadi muonekano kiafrika zaidi katika video zake. Nyimbo alioiachia awali kwa jina “Oh my gosh” imeweza kupokelewa vyema barani na nje ya nchi na kumfanya bado awe ni msanii alie wapiku wasanii wenziwe wa jinsia yake, nchini Nigeria hadi kimataifa zaidi.

Yemi Alade ameweza kuachia video yake akiingia studioni na Nyota wa marekani wa mziki wa Rap Rick Ross aka Rozzay pamoja na kuonekana wakipongezana kwa kazi walioifanya. Masaa ya kupindua siku baadae Yemi aliweza kuachia Video yake mpya ambayo ni (Remix) aliomshirikisha Staa huyo wa Marekani ili kuwa kosha mashabiki zake zaidi kwa kuwa dondoshea mzigo mpya ambao wengi hawakutarajia. Kitu ambacho hata Diamond platnumz alipofanya kazi na Rick Ross wengi walibaki mdomo wazi ma wengine kuponda kiushabiki zaidi kwa sababu hakikuwa kitu cha kawaida kwa msanii wa Afrika mashariki baada ya miaka kadhaa iliyopita iliyo waleta karibu Msanii Alikiba na bingwa wa RnB Robert Kelly aka R.Kelly katika project yao One 8 miaka kadhaa iliyopita.

View this post on Instagram

watch.

A post shared by Soundcity Africa (@soundcityafrica) on

Kulingana na sanaa ya sasa ilivyopanda na kuonekana wasanii wengi wa kiafrika kukaza buti katika sanaa yao, hii imewavutia wasanii wengi ambao ni maarufu mabara mengine kuja kujichanganya nao ili wapate kuongeza duara lao la mashabiki barani Afrika pamoja na kubadili ladha tofauti kiubunifu katika mziki wao. Yemi Alade sasa amiachia rasmi kazi hiyo ambayo inatarajiwa kuuwasha moto mkali sana kwenye chati za Nigera na kote barani Afrika hadi kimataifa zaidi kufikia mabara mengine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Like Us on Facebook

Copyright © 2020 Mgahawani Media.