Connect with us

Sports

Neymar apokea adhabu ya mechi 3 dhidi ya UEFA

Published

on

Kwa mujibu wa shirika kuu la mchezo wa soka barani ulaya, imeamua kumpa adhabu nyota huyo ambae ni Raia wa Brazil anaeichezea klabu ya PSG nchini Ufaransa. Hii imesababishwa na maamuzi aliyoyatumia kiushabiki zaidi, kipindi ambacho alikuwa nje ya uwanja akiwa na majeruhi wakati tumu yake ilipokutana ana kwa ana na klabu ya Manchester United. PSG ilipokutana na klabu hiyo maarufu kutokea nchini Uingereza kwenye hatua ya mtoano wa 16 bora kwenye ligi kuu ya mabingwa Barani Ulaya, wakati ilipoichapa mabao mawili bila (0-2) nyumbani kwao Mancester United pale Oldtrafford na kuja kuruhusu kizembe, magoli matatu kwa moja (1-3) dimbani kwao Park Des Princess nchini Ufaransa.

Mchezaji wa Paris Saint Germain, Neymar anakabiliwa na adabu ya kukosa mechi 3 za Ligi ya mabingwa Barani ulaya.

Mnamo Mei tarehe 6 ilikuwa siku ambayo Mabingwa hao wa Ufaransa kuishangaza dunia na kuwafanya Manchester United kutamba kifua mbele pamoja na kujipa matumaini lukuki ya kuwania kwakina kinyang’anyiro cha kombe hilo tangu wachukue ubingwa huo mwaka 2008 kabla kutolewa na wababe wa ligi hiyo Fc Barcelona. Neymar anakabiliwa na tuhuma za kuposti ujumbe uliosheheni povu na hasira baada ya klabu yao kukatishwa matumaini ya kufuzu hatua hiyo ya 16 bora, pindi muamuzi alipowaadhibu kwa kupeana penalti katika dakika za mwishoni mwa mechi hiyo. Kitendo hicho kilionekana kumkera sana Neymar aliye kuwa akitazama mechi nje ya uwanja huo na kuandika “There is no penalty. How can it be a handball when it hits his back! Go **** yourselves!” kitendo hicho cha kuanika maneno hayo ya jadhba, yameikasirisha shirkika la UEFA na kuwafanya waamuzi hao kufikia hatua ya kumpa adhabu hiyo ya kukosa mechi tatu za Bara Ulaya.Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Like Us on Facebook

Copyright © 2020 Mgahawani Media.